Aliyekuwa rais wa Interpol akataliwa rufaa na mahakama nchini Afrika ya Kusini.
Pretoria, Afrika ya Kusini - 03/12/2011. Aliyekuwa mkuu wa polisi nchini Afrika ya Kusini amekataliwa rufaa yake aliyo kata kutokana na hukumu aliyo pewa na mahakama kwa kuhusika na katika bishara ya madawa ya kulevya.
Jackie Selebi 61, ambaye alishawahi kufanya kazi na interpol, alikutwa na hatia ya kuhusika katika biashara hiyo na kuhukumiwa kwenda jela kwa muda wa miaka 15.
Mwanasheri Wynanda Coetzee ambaye anamwakilisha Jackie Selebi alisema " Selebi hajiwezi na kwa sasa yupo hospitali na hakuweza kueleza lolote kutoka na hali yake."
Jackie Selebi ambaye ni mmoja ya wapigania haki zidi ya ubaguzi wa rangi wakati wa serikali ya kibaguzi enzi za harakati za kupambana na ubaguzi wa rangi nchini Afrika ya Kusini.
George Bush ziarani Afrika kupambana na ukimwi.

Dar es Salaam, Tanzania - 03/12/2011. Aliyekuwa rais wa Marekani George Bush yupo ziarani katika bara la Afrika katika juhudi zake za kupambana na ugonjwa wa ukimwi.
Nchia ambazo anazotembelea ni Tanzania, Zambia na Thiopia.
Akiwa nchini Tanzania rais huyo wa zamani wa Marekani alitembelea sehemu mbali mbali na hasa katika vitu vinavyo shughulikia kupambana na ugonjwa wa ukimwi.
Goerge Bush alisema " Watanzania mmeonyesha mfano katika harakati za kupambana na ukumwi na Wamarekani watazidi kushirikia na Watanzania kuhakikisha ugonjwa huu unashindwa."
George Bush katika ziara yake barani Afrika ameambatana na mkewe Laura Bush.
No comments:
Post a Comment