Rais wa zamani wa Ufaransa Jacques Chirac ahukumiwa miaka miwili.
Paris, Ufaransa - 16/12/2011. Mahakama nchini Ufaransa imemuhukumu aliyekuwa raia wa Ufaransa kifungo cha miaka miwili baada ya kukutwa na kosa la kuhusika katika njama za rushwa na kuwepo na matumizi yasiyo elewaka.
Jacques Chirac amehukumiwa kifungo cha nje cha miaka miwili, na kuwa kiongozi wa pili kufuatia kesi ya Philippe Petain iliyo tokea wakati wa vita pili vya dunia.
Hukumu hiyo ilitolewa bila Jacques Chirac kuwepo mahakamani kutokana na hali yake ya kifya kutoruhusu kuwepo mahakamani.
Luis Moreno Ocampo atatitwa na vifo vya Gaddafi na mwanae.

Ze Hague, Uhollanzi - 16/12/2011. Mwanasheria mkuu wa mahakama ya inayo shughulika na kesi za jinai na kutetea haki za binadamu ya Uhollanzi amedai ya kuwa mauaji ya rais wa Libya Muammar Gaddafi na mwanaye, yalikiuka haki za binadamu na kuna kesi ya kujibu kwa wale walio husika na mauaji hayo.
Luis Moreno Ocampo alisema " kutokana na jinsi walivyo uwawa Gaddafi an mwanaye, kuna leta
wasiwasi ya kuwa mauaji hayo yalifanyika kwa kuvunja sheria na kuna haja ya kuchunguzwa."
Nimetuma barua kwa serikali ya mpito ya Libya na kutaka waaanze uchunguzi na kama wakishindwa kufanya hivyo basi itabidi tufanye uchunguzi wetu wenyewe." aliongezea Ocampo.
Tamko hilo la Ocampo limefuatia ombi la mtoto wa Muammar Gaddafi Aisha Gaddafi, kutaka kifo cha baba yake kichunguzwe.
Urussi yajiunga na shirika la bishara la Kimataifa.

Geneve, Uswisi - 16/12/2011. Shirika la biashara la Kimataifa World Trade Organization - WTO ilimepitisha na kukubali kujiunga uanachama kwa nchi ya Urussi kwenye shirika hilo.
Olesugun Aganga waziri wa biashara wa Nigeria na ambaye nimwenyekiti wa kikao cha nane cha shirika hilo aliwatangazia wajumbe kwenye kikao hicho ya kuwa Urussi kuanzia sasa itakuwa mwanachama wa shirika hilo.
Kufuatia kujiunga huko kwa Urussi kwa shirika hilo, " Urussi itakuwa inanunu vitu kutoka nchi za jumuiya ya Ulaya kwa bei nafuu na kuweza kuuza mafuta na gasi bila matatizo yoyote kwa nchi hizo."
Waziri mkuu wa Urussi, Vladimir Putin alisema " kufikiwa makubaliano hayo ni matokeo ya mazungumzo yaliyo chukua muda na washiriki wenzetu."
Urussi imekuwa mwana chama wa WTO kufuatia mazungumzo yaliyo chukua miaka 18.
No comments:
Post a Comment