Saturday, December 31, 2011

Marekani na na nchi za UAE zakubaliana kikataba ya kiulinzi.

  Marekani na na nchi za UAE zakubaliana kikataba ya kiulinzi.


Washington, Marekani - 31/12/2011. Serikali ya Marekani na umoja wa shirikisho wa nchi za Kiarabu United Arab Emarates zimekubaliana kuwekwa mitambo ya kiulinzi katika nchi za UAE.
Makubaliano hayo ambayo yalisainiwa 25/12/2011,  yatiwezesha Marekani kuweka mitambo yake ya ulinzi katika nchini hizo.
Msemaji wa serikali George Little alisema "mkataba huo ambao utagharimu kiasi cha dola za Kimarekani $3.48billion na itasidia kuimarisha ulinzi katika nchi hizo."
Mkataba huu utawezesha kuwekwa kwa mitambo ya kuzuia mabomu, mitambo ya mashabulizi 96, rada na mitambo mingine ya kiulinzi.
Marekani na umoja wa shirikisho wa nchi za Kiarabu zimekuwa na uhusiano wa karibu kwa muda mrefu jambo ambalo limeziwesha nchi hizi mbili kushirikiana katika maswala ya kiuchumi na kiulinzi.

 Jeshi la  Ethiopia laingia nchini Somalia.

 Beledweyne, Somalia - 31/12/201Jeshi la Ethiopia limefanikiwa kushikiria mji wa Beledweyne kutoka mikononi mwa kundi la Al-Shabab.
Kundi la Al Shabab limedai kuyaondoa majeshi yake katika eneo hilo baada ya kuzingirwa na jeshi la Ethiopia.
Kwa mujibu wa wanchi waliona  wanajeshi wa Ethiopia walisema  " tumeona magari ya kijeshi yakizunguka zunguka hapa mjini tangu jana."
Habari kutoka jeshi la Ethiopia zinasema "jeshi la Ethiopia limeamua kuisaidia Somalia baaday ya serikali hiyo ya Somalia kuomba msaada."
Wakati huo huo habari kutoka ofisi ya  waziri mkuu wa Somalia zinasema " serikali ya Somalia imetangaza ukombozi na kuhaidi kupambana na kundi la Al-Shabab kwa kila hali na tutaomba kila msaada kwa nchi majirani ili tuweze kulinada nchi yetu na kuliangamiza kundi la Al-Shabab."
Kundi la Al-Shabab limekuwa likipambana na serikali ya Somalia kwa muda mrefu jambo ambalo limeifanya serikali kushindwa kufanya shuighuli zake za kusaidia wananchi na kuijenga nchini.

Kim Jong Un ateuliwa rasmi kuwa kiongozi wa Korea ya Kaskszini.

 Pyongyang, Korea ya Kaskazini - 31/12/2011. Mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Korea ya Kaskazini Kim Jong Il ambaye amefariki dunia siku chache zilizo pita ameteulia kushika madaraka ya baba yake.
Kim Jong Un ambaye aliongoza mazishi ya baba yake na kuhusishwa na maswala ya serikali kabla ya baba yake Kim Jong Il kufariki ameteuliwa rasmi kuwa kiongozi wa chama tawala cha wafanyakazi ana ambacho ndoyo kinacho ongoza nchini hiyo.
Kuteuliwa huko kwa Kim Jong Un atakuwa kiongozi wa jeshi na kuwa na madaraka ya juu katika nchi hiyo.
Kwa mujibu wachunguzi wa mambo ya kisiasa na maswala ya ulinzi wanadai huenda  mrithi huyo akawa mgumu  kushirikiana naye kwa kuzingatia ya kuwa amezungukwa na watu waliokuwa wanafanya kazi na baba yake.

No comments: