Friday, December 30, 2011

Rais Hugo Chavez atilia wasiwasi Marekani kuhusu kuugua ugonjwa wa tarasini-kansa.


Marekani yaiuzia Saudi Arabia ndege za kijeshi.

Riadhi, Saudu Arabia - 30/12/2011. Marekani imeiuzia serikali ya Saudi Arabia ndege za kivita  zenye thamani ya dola za Kimarekani 30 billion.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani  Josh Earnest alisema "makubaliano hayo yatawezesha kupatikana kwa kazi wa watu 50,000 ."
Ndege hizo aina ya  Jet F-15s  ziliuzwa ikiwa ni moja ya makubaliano ya kibiashara kati ya Saudi Arabia na Marekani.
Andre Shapiro ambaye ni mmoja ya maofisa wa Ikulu ya Marekani alisema " kuuzwa kwa ndege hizo nchini Saudi Arabia ni kutoa onyo kwamba Marekani itafanya kila njia kuleta amani katika eneo la Mashariki ya Kati na itasaidia nchi hiyo kuwa imara..
Habari za kuuzwa kwa ndage hizo zimepatika baada ya rais Baraka Obama kuyasema hayo katika mji wa Hawaii ambapo yupo huku huko kwa mapumziko.

Rais Hugo Chavez atilia wasiwasi Marekani kuhusu kuugua ugonjwa wa tarasini-kansa.

Karakas, Venezuela - 30/12/2011. Rais wa Venezuela ametilia wasiwasi ya kuwa Marekani inashiriki katika kuwaambukiza ugonjwa wa saratani viongozi wanaonekana kupingana na mwenendo wa nchi Ya Marekani.

Rais Hugo Chavez  57 alisema " nisingependa kusababisha mfarakano lakini inawezekani Marekani ina husika katika kuwaambukiza ugonjwa wa saratani - kansa viongozi wa Amerika ya Kusini ambao tunapingana na nyendo za kibepari za Marekani." 
" Ikiwa Marekani inafanya kitendo hiki itakuwa ni cha kushangaza, na kitajulikana tu, kwani 1946-48 walifanya majaribio kwa watu wa Guatemala na matokeo yake watu walipata magonjwa ya siri, na haya yalikuja julikana miaka 50 baadaye."
"Nimeamua kusema hivyo ili kuweka mfahamo wangu wazi na nasema haya kutumia uhuru wangu niliyo nao," aliongezea rais Hugo Chavez.
Hata hivyo serikali ya Marekani imekanusha maoni hayo, msemaji wa serikali  Victor Nuland alisema "maoni kama hayo ni ya kushangaza,  haya na msingi wowote na siyo ya kuthaminika." 
Matamshi hayo ya rais Hugo Chavez yamekuja baada ya rais wa Argentina Cristina Fernandez Kirchner 58 kujulikana ya kuwa anaugonjwa wa tarasini - kansa, huku rais wa Paruguayi Fernando Lugo 60, rais wa Brazil Dilma Rousseff 64 na rais mstaaf Luiz Inacio Lula da Silva kutibiwa  ugonjwa wa tarasini - kansa.
Rais Hugo Chavez aliyaongea hayo kwa kuangalia mfululizo wa kuugua ugonjwa wa tarasni - kansa kwa viongozi hawa wanao pingana na Marekani na kudai ya kuwa rais mstaafu wa Kuba amekuwa akimwonya juu ya mwenendo wa vyakula  anavyo kula kwani vinachangi katika kuambukizwa ugonjwa wa tarasani - kansa.

Wafanyakazi wa shirika la waganga wasio na mipaka wauwawa nchini Somalia.

Mogadishu, Somalia - 30/12/2011. Mtu  mmoja amewashambulia  na kuwauwa wahudumu wanaotoa misaada wa shirika la waganga aliopo nchini  Somalia.
Mauaji hayo yalitokea kwenye ofisi za waganga hao wasiti na mipaka Medicins Sans Frontieress wahudumu.
Waziri wa mambo ya ndani wa Somalia Abdisamad Moalin Mahamud alisema " mtu huyo ambaye aliwauwa wafanyakazi wa shirika baada ya kufukuzwa kazi kutoka shirika hilo."
"Mtu huyo aliye fanya kitendo hiki ni mtu ambaye amekuwa anafanya kazi kwa muda mrefu katika mashirika ya misaada." aliongezea waziri Abdisamad.
Kwa mujibu wa habari zilizo patikana zinasema "watu ambao wamepoteza maisha yao ni rais wa Belgium Philippe Havet 53 na Andrias Karel Keiluhu  44 raia wa Indonesia."
Kufuatia mauaji hayo serikali imeaanza uchunguzi wake na kuimarisha usalama zaidi kwa wafanyakazi wa shirika hilo la waganga wasio na mipaka  waliopo nchini humo.

Alqaeda yatuma wapiganaji nchini Libya.

Tripol, Libya - 30/12/2011. Kiongozi wa kundi la Alqaeda ametangaza ya kuwa ametuma mmoja wa wapiganaji wa kundi hili nchini Libya ili kuunda kikundi imara.
Kwa kujibu wa habari kutoka kwa kundi hili zimasema " Ayman al Zawahiri amemtuma mpiganaki huyo ambaye hapo awali alikuwa  amekamatwa  na kuwekwa chini ya ulinzi nchini Uingereza."
Mpiganaji huyo aliingia nchini Libya mwezi wa tano baada ya kiongozi huyo wa Libya kuona ya kuwa Muammar Ghaddafi amesha poteza uwezo wa kuongoza nchi."
Hadi sasa inaaminika yakuwa mpiganaji huyo ameshawakusanya wapiganaji 200 kwa mujibu wa wachunguuzi  wa mambo ya usalama.

No comments: