Palestina yakubaliwa kujiunga na UNESCO

Paris, Ufaransa - 14/12/2011. Serikali ya Wapalestina imeongezwa kuwa mwanachama wa UNESCO -UN Education, Scientific and Cultural Organasation, katika sherehe iliyo fanyika nchini Ufaransa baada ya bendera ya Wapalestina kupandishwa juu sambamba na bendera ta umoja wa mataifa kama ishara ya kujiunga na shirika hilo.
Rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas alisema " hii ni historia na tunatumaini yakuwa Wapalestina watakuwa wanachama wa mashirika mengi muda si mrefu."
Kukubaliwa huko kwa Wapalestina kujiunga na UNESCO kumekuja huku viongozi wa nchi hiyo wakiwa katika kampeni ya kutaka Wapalestina watambulike rasmi katika baraza la umoja wa mataifa kama taifa huru.
Pakistani yazidi kuiwekea ngumu Marekani kusafirisha vifaa nchini Afghanistan.

Islamabad, Pakistan - 14/12/2011. Serikali ya Pakistan imetangaza ya kuwa vikwazo na vizuizi zidi ya vifa vya kijeshi na vya ujenzi vitaendelea hadi hapo hali ya mapatano itakapo fikiwa.
Waziri mkuu wa Pakistani Yousuf Gilani alisema "kwa sasa kuna kuto kuaminiana kati ya Marekani na Pakistani jambo ambalo linaleta wasiwasi kwa pande zote na ikiwa hali itazidi kuwambaya basi itabidi tufunge mawasiliano ya anga."
Uhusiano wa Marekani na Pakistani uliingia dosari baada ya askari 24 wa Pakistani kuuwawa kutokana na shambulizi yaliyo fanywa na jeshi la Marekani.
Rais Baraka Obama awakaribisha wanajeshi kutoka Irak.

Baraka OBama alisema "ningependa kusema ya kuwa tumefikia mwisho wa vita vya Irak na karibuni nyumbani na Irak sasa ipo chini ya Wairak na hongereni kwa kazi nzuri kwa kuiweka Irak katika hali ya kuweza kujijenga."
Naningependa kuwahakikishia ya kuwa ifikapo mwisho wa mwezi huu Desemba wanajeshi wote wa Marekani watakuwa nyumbani." Aliongezea rasi Obama.
Kuwasili huko kwa wanajeshi hao kunafikia tamati baada ya vita vya kuingoa serikali ya aliye kuwa rais wa Irak Sadaam Hussein mwaka 2003.
No comments:
Post a Comment