Nchi za Umoja wa Ulaya zaamua kuimarisha sarafu ya Euro na kuicha Uingereza.

Brussels,Belgium - 09/12/2011. Mkutano uliyo fanyika ili kuimarisha sarafu ya Euro umemalizika huku Uingereza kukataa kutia sahini mkataba wa kudhibiti mahesabu na matumizi ya nchii wanachma wa jumuia hiyo.
Mkutano huo ambao ulizikutanisha nchi wanachama wa jumuia ya Ulaya, ulikuwa na madhumuni ya kuweka sheria ya kudhibiti matumizi na mipangilio ya kifedha kwa nchi wana chama ili kuzuia mporomoko wa kiuchumi usitokee tena.
Kufuatia uamuzi huo wa Uingereza kuto tia sahini mkataba huo, nchi nyingine zilikubaliana na sheria hiyo na kuifanya Uingereza kuwa nchi pekee katika jumuia hiyo yenye nchi 27 kutokubaliana na mpango huo.
Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron alisema " nimeamua kuto sahini mkataba huo baada kuona ya kuwa hatainufaisha Uingereza."
Hata hivyo rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy alisema " hatukuweza kukubaliana na matakwa ya Uingereza na hivyo nchi ambazo zilizomo kwenye jumuia na zinazo tumia sarafu ya Euro zitaendelea na mswada huo ili kuimarisha nguvu ya sarafu hii."
Kwa mujibu wa wataalamu wa mambo ya kidiplomasia wameseama " uamuzi wa Uingereza kukataa kusahini mkataba huo kutaifanya Uingereza kutengwa, hasa ifikapo katika maamuzi ambayo yanazigusa nchi zilizo kubaliana na mswaada huo."
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa awasili nchini Somalia.

Ban-Ki-moon alifanya ziara hiyo ya ghafla nchini Somalia na kuwa ni kiongozi wa kwanza wa Umoja wa mataifa kuwasasili nchini humo tangu kuanza vurugu za kisiasa mwaka 1991.
Katibu huyo wa Umoja wa Mataifa alisema "ofisi za umoja huo zilizopo nchini Kenya zitahamia nchini Somalia na nimuhimu ilikuleta uaminifu kwa wananchi wa Somalia."
Kuwasili huko kwa Ban Ki-moon kumekuja baada ya jeshi la Umoja wa Afrika kuweza kushikilia maeneo tofauti yaliyopo nchini Somalia.
Katika ziara hiyo Ban Ki -moon alipokelewa na waziri mkuu wa Somalia Abdeiweli Mohamed Ali.
No comments:
Post a Comment