Thursday, December 29, 2011

Iran na Marekani zavutana kwa maneno juu ya ghuba ya Strait Hormoz

Maharamia wa Kisomali wateka meli nyingine tena.

Mogadishu, Somalia - 29/12/2011. Maharamia wa Kisomalia wameteka nyara meli ya mizigo na wafanyakazi 18 karibu na pwani ua Oman.
Kwa mujibu wa habari zilizo patikana kutoka ofisi za mkurugenzi wa meli ya India zinasema "meli hiyo Turkey-bound Enrico levoli  wenye wafanyakazi kutoka India 7, Itali 6, na watano kutoka Uikraine ipo njiani kuelekea pwani ya Somalia na meli hiyo ilikuwa imebeba caustic soda kutokea Iran kwenda Uturuki."
Utekwaji wa nyara huo umekuja wakati inaaminika ya kuwa maharamia hao wamekuwa nawakati mgumu wa kuteka nyara meli kutokana na ulinzi unao tolewa na majeshi ya majini ya nchi za Ulaya.
Handi kufikia sasa inaaminika kuna  idadi wa watu 200 bado wanashikiliwa na maharamia baadaya kuteka meli walizo kuwa wakifanya kazi.

Hamid Karzai aweka masharti ya kufunguliwa ofisi za Taliban nchini Katar.

Kabul, Afghanistan - 29/12/2011. Rais wa Afghanistan amekubali kufunguliwa ofisi za kundi la Taliban nchini Katar ikiwa zitakuwa kwa mazumuni ya kuleta mafanikio ya mazungumzo ya amani.
Rasi Hamid Karzai alisema "Kama Marakani inasisitiza kufunguliwa kwa  ofisi za Taliban tutakubaliana ufunguzi wa ofisi hiyo nchini Katar kwa malengo ya kuwa itatumika katika kujenga uhusiano wa kuleta amani kati yetu japo inasikitisha."
Msukumo huo wa kuleta mazungumzo ya amani na kundi la Taliban umekuwa na mvutano hasa baada ya kujulikana ya kuwa ifikapo 2014 jeshi la Marekani litaondoka rasmi nchini Agahanistan.
Hata hivyo serikali ya Afghanistan imekuwa na wakati mgumu wa kufanya mazungumzo na kundi la Taliban kutokana na historia ya kundi hilo.

 Korea ya Kaskazini kumaliza rasmi leo msiba wa kiongozi wao Kim Jong Il. 



Pyongyang, Kora ya Kaskazini - 29/12/2011. Maelfu ya wanchi wa Korea ya Kaskazini  wameshuhudia mwili wa aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Il ukipitishwa kwenda kwenye maziko.
Mwili wa Kim Jong Il 69, ulipitishwa kwenye gari aina ya remozini na kuongozwa na mwanae Kim Jong Un huku wanajeshi wakiwa wamejipanga barabarani kumwaaga kwa mara ya mwisho.
Seo Ju-rim mmoja wa wanajeshi walioudhuria mazishi yaho alisema " kwa kuangalia kuanguka kwa barafu kunanifanya nimkumbuke kiongozi wetu mpenda nchi ambaye alikuwa anaongoza kwa upendo na ameicha nchi yetu ikiwa na nguvu zaidi."
Wasemaji wa maswala ya hali ya Korea ya Kaskazini waliopo nchini Korea ya Kusini walisema " mazishi ya Kim Jong Il yanafanana na  mazishi alioyo fanyiwa baba yake Kim Il Sung mwaka 1994.
Kufuatia kifo cha Kim Jong Il, mtoto wake Kim Jong Un 28, amekabidhiwa kiti cha baba yake kuiongozi nchi hiyo.
Iran na Marekani zavutana kwa maneno juu ya ghuba ya Strait Hormoz.

Tehran, Iran 29/12/2011. Makamu wa rais wa Iran ametishia ya kuwa Iran itafunga ghuba ya Strat Hormuz ikiwa vikwazo vya kiuchumi zidi ya Irani vitaendelea.
Makamu wa rais Mohamed Reza Rahimi alisema " hakuna mafuta yatakayo ruhusiwa kupita katika eneo la Strait Hormuz, na siyo  niya yetu kufanya hivyo, lakini ipo haja ya kufanya hivyo ili tuweze kutuma ujumbe kwa wale wanao fikiria kufanya hivyo na wao waone ugumu wa vikwazo na waache kuweka vikwazo."
Hata hivyo msemaji wa jeshi la Marekani  Navy 5th  Rebecca Rebarich alisema " hatutaweza kukubali hali hiyo itokee ya kuzuiwa mafuta yasipite kwenye eneo la Strait Hormuz na tupo tayari kulinda eneo hilo ili kuhakikisha mafuta yanapita bila shida."
Malumbano hayo yamekuja wakati Iran inafanya mazoezi ya kivita karibu na eneo hilo.

Mahakama nchini Urusi  yakataa kukifungia kitabu cha Hare Krishna.

Tomsk, Urusi 29/12/2011- Mahakama nchini Urusi imekataa kukifungia kitabu cha dini ya Hare Krishna, baada ya madaya yakuwa kitabu hicho kinapotosha maadili ya watu.
Uamuzi huo wa mahakama ulipokelewa na kushukuriwa na ofisi ya waziri wamabo ya nje wa India kwa  kusema " swala kama ili nyeti limeamuliwa  kwa kufuata misingi yeti na nifuraha." 
Akiomba kufugiwa kwa kitabu hicho mwanasheria wa serikali alidai "kitabu hicho likicho tafsiliwa kwa Kirusi 'Bhagavad Gita kinapotosha na kutangaza maadili mabaya kwa wale wasio waumini na vina itikadi kali."
Hata vivyo mahakama ilkataa maombi ya mwanasheria huyo.
Kesi hiyo iliyo anza mwezi wa June mwaka huu.

India na Japan wakubaliana kubadalishana pesa.


New Delhi, India - 29/12/2011. Serikali za India na Japani zimetiliana sahii mkataba wa kibiashara na kukubaliana kukubadilishana fedha za nchi hizo.
Mkataba huo ambao utaziwezesha nchi hzo kubadilishana kiasi cha dola 15billion.
Waziri mkuu wa Japan Yoshihiko Noda alisema " mkataba huu utasidia kuimarisha uchumi wanchi hizi mbili."
Naye waziri mkuu wa India Manmohan Singh alisema " nimefurahi kutaokana na kukubaliana na waziri mkuu Noda."
Kufuatia makubaliano hayo Japan itaweza kuiazima India pesa ili iweze kulinda thamani ya  peas ya India  ijulikanayo kama Repee.

Mjumbe wa nchi za Kiarabu aliyepo Syria atoa maono ya mwanzo kuhusu hali ilivyo. 
Homs,Syria -29/12/2011. Mmoja wa wajumbe wanaoakagua hali ilivyo nchini Syria kutokana na vurugu za kisiasa na ambaye raia wa Sudan  ameongelea hali ilivyo hadi sasa nchini Syria.
Jenerali Mohamed Ahmed Mustafa al Dabi alisema "ingawa sehemu nyingine zilikuwa za kuoesha yakuwa kulikuwa na machafuko, lakini tulivyo fika maeneo mengi hayukuonekana kutisha na hali ilikuwa shwali na hatukuona vifaru vya jeshi ili tuliona gari za jeshi, na ningependa mkubuke ya kuwa hii ilikuwa siku ya kwaza  tangu tuanze uangalizi wetu."
Hata hivyo maoni ya Jenerali Dabi yalitiliwa wasiwasi na  nchi za Magharibi kwa kusema ya kuwa maoni ya ke ni ya mwazo tu."
Nazo habari kutoka ofisi za umoja wa nchi za Kiarabu zilisema, "maoni ya Jenerali Mohamed Mustafa Dabi yanathaminika kwani ni muhimu kwa kuzingatia yeye nimwanajeshi na mwana diplomasia vilevile."
Syria imetembelewa na wakaguzi 50 wa nchi za jumuiya ya Kiarabu, ili kutathmini hali halisi ya matatizo ya kisiasa yanayo endelea nchini humo.

No comments: