Tuesday, July 26, 2011

Baraka Obama awasihii viongozi wenzake kukubalia

Baraka Obama awasihii viongozi wenzake kukubaliana.
Washington, Marekani - 26/07/2011. Rais wa Marekani amelitangazia taifa na kuonya ya kuwa kama hakutawa na makubaliano itahatarisha uchumi na maisha ya jamii kwa ujumla.
Rais Baraka Obama alisema " hali hii siyo nzuri kwa kuendelea kulumbana kwani hakutasaidia na matokeo yake yatalitia taifala Mareani katika hatari ya kuporomoka kiuchumi na maisha ya wanchi wa Marekani, kwani hali hii haijawahi kutokea hadi kulipelekea taifa kufikia hali hii."
Rais Obama alihutubia taifa baada ya kutofikia makubaliano kati ya chama chake cha demokrasi kilichopo madarakani na chama cha wapinzani cha repablikani ambacho inapinga miswada ya ambayo inatolewa na serikali.
Umoja wa mataifa waongeza nguvu kupambana na baa la njaa.
Rome
, Itali -26/07/2011. Shirika lainalo shughulikia maswala ya chakula duniani , limepitisha mswaada wa kuanza kusambaza chakula kwa kutumia usafiri wa ndege kati nchi ambazo zimekumbwa na ukama katika eneo la Afrika ya Mashariki.
Habari zinasema " kazi hiyo ya kuanza kusambaza chakula katika maeeneoa hayo itaanza mapema hivi karibuni ili kukabili baaa hilo la njaa na kwa kuzingatia watoto ndiyo walioathirika kwa kiasi kikubwa." Lilisema shirika hilo.
Uamuzi huo umekuja baada ya mkutano uliofanyika nchi Itali ambao ulikuwa na mazumuni ya kupanga mbinu za kupambana na baaa hilo.
Nchi ambazo zinakabiliwa na baaa hilo ni Djibouti, Ethiopia, Kenya, Somalia, Sudan na Uganda.

No comments: