Friday, July 22, 2011

Mabomu yalipuka na kuleta maafa nchini Norway.

Mabomu yalipuka na kuleta maafa nchini Norway.
Aslo, Norway 22/07/2011. Jiji la Olso limekutwa na mshituko baada ya mabomu kulipuka katika ofisi za serikali na kusababisha maafa makubwa kwa jamii na raia.
Waziri mkuu wa Norway Jens Stoltenberg ambaye inasemekana hakuwepo katika ofisini wakati wa milipuko hiyo yupo salama.
Hata hivyo waziri mkuu ambaye alitakiwa kuhudhulia mkutano wa umoja wa vijana wa chama cha Labour ambao ulikuwa unafanyika katika kisiwa kilichopo nje kidogo ya mji wa Aslo mbapo kulitokea mashambulizi ya risasi katika kambi hiyo, baada ya mtu mmoja kuvaa nguo kama polisi kuanza kushambulia katika kambi hiyo na kuleta maafa makubwa na kupoteza maisha ya vijana waliokuwa kwenye mkutano huo..
Hadi kufikia sasa hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na mashambulizi hayo na idadi ya watu waliopoteza maisha na kujeruhiwa katika matukio hayo mawili bado haijajulikana na polisi wanaendelea na uchunguzi.
Ugiriki yapata mkopo kwa mara yapili.
Brussels, Ubeligiji-22/02/2011. Viongozi wa nchi zinazo tumia sarafu ya Euro wamekubaliana kwa pamoja kuta mkopo kwa serikali ya Ugiriki ili iweze kujikwamua kiuchumi ambao ulikwa unaelekea kuporomoka.
Mkutano huo ulio washirikisha viongozi na wafanyabiasha wa sekta binafsi walifikia makubaliano na kuamua kuikopesha Ugiriki kiasi cha euro 109 billion ambazo ilikuwa inazihitaji ili kuinua na kuimarisha uchumi wake.
Kwamujibu wa habari zinasema , "kwenye mkutano huo viongozi wa serikali waliwashawishi viongozi wa mabenki kukubali kupokea hasara ili kuiokoa Ugiriki kiuchumi."
Ugiriki imebidi ipewe mkopo kwa mara pili baada ya mkopo wa kwaza kutotoshereza kuimarisha uinuaji wa uchumi wa nchi hiyo.
Kundi la Al Shabab lapinga kusambazwa kwa chakula nchini Somalia.
Mogadishu
, Somalia -22/07/2011. Kundi la la Al Shabab linalo pingana na serikali ya Somalia, limekataaa kuruhusu mashirika ya kimataifa yanayo toa msaaada wa chakula kuingia katika maeneo linalo miliki na kudai ya kuwa hakuna njaa ya kutisha kama inavyo tangazwa.
Habari kutoka kwa kundi hilo zimesema " hatutaruhusu kwa kundi lolote kuingia katika maeneo yetu kwa sababu za kusambaza chakula, kwani madi hayo siyo ya kweli na wala hakuna shida ya njaa kama inavyotangazwa."
Al Shabab kundi ambalo hapo awali lilikubali kutoa ruhusa kwa mashirika ya kimataifa kusambaza chakula katika maeneo inayo yashikilia, imeamua kubadisha uamuzi huo ambao hadi sasa unawashangaza wahudumu na wahisani wanao sambaza na kutoa msaada wa vyakula katika nchi ya Somalia ambayo imekumbwa na ukame na kufikia kutangazwa na umoja wa mataifa kuwa nchi hiyo imekumbwa na baaa la njaa la kihistoria katika kipindi cha miaka 60.

No comments: