Sunday, July 3, 2011

Hezbollah yalia na Izrael katika mauaji ya Rafik Hariri.

Ugiriki yapata mkopo.
Athens, Ugiriki -03/07/2011. Serikali ya Ugiriki imepatiwa mkopo wa pesa za dola ya Kimarekani zipatazo Billlion 18 kutoka kwenye jumuya ya Ulaya.
Wakipitisha muswada huo, mawaziri wa fedha wa jumuya hiyo walikubaliana kwa pamoja kuipa Ugiriki fedha hizo baadaya serikali ya Ugiriki kukubali kufanya mabadiliko katika sera zake za kuijenga nchi hiyo kiuchumi.
Vilevile jumuya Ulaya imewaagiza viongozi wa siasa wa Ugiriki kushirikiana kikamilifu ili kuinua hali ya uchumi wa nchi hiyo.
Hezbollah yalia na Izrael katika mauaji ya Rafik Hariri.
Beirut, Lebanon -03/07/2011. Kiongozi wa kundi la Hezbollah ameilaumu Izrael kwa kuhusika na mauaji aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon Rafik Hariri mwaka 2005.
Hassan Nasrallah alisema " tunajua Izrael imehusika katika mauaji na hii kesi iliyopo nikwaaajili ya kuleta mvurugano wa kisiasa nchini Lebanon na tunaomba kati hiyo ifanye uchunguzi wake kwa upande wa Izrael pi
na siyo kuleta mvurugano kati ya Walebanon.
Rafik Hariri aliuwawa baada ya mlipuko wa mabomu kulipuka katika eneo alilo kuwepo na tangu kipindi hicho cha kifo chake, serikali ya Lebanon imekuwa ikitafuta kwanundani nani aliye husika na kifo chake.
Ethiopia yakumbwa na ukame mkubwa.
London,
Uingereza -03/07/2011. Serikali ya Uingereza imehaidi kutoa msaada wa pesa kiasi cha paundi million 38 kwa serikali ya Ethiopia ili kusaidia kununua chakula, baada ya nchi hiyo kukumbwa na ukame mkubwa.
Waziri wa ushirikiano wa kimataifa wa Uingereza Andrew Mitchell alisema " msaada hun wa pesa utaambatana na mpango wa shirika la chakula duniani katika kukuza kuwepo kwa lishe bora kwa watoto wapatao 329,000."
Ethiopia nchi mojawapo katika bara la Afrika ambayo imekumbwa na ukame wa hali ya juu kwa kipindi cha miaka 60 iliyopita.Hata hivyo nchi hiyo ilikumbwa na ukame kwenye miaka ya themani ambapo dunia nzima ilishikwa na mstuko mkubwa.
Kwamujibu wa habari kutoka shirika la umoja wa mataifa zinasema "nchi nyingine ambazo zinakabiliwa na hatari hiyo ya ukame ni Somalia, Djibouti na Kenya."