Wednesday, July 20, 2011

Wanchi wa Malawi waandamana.

Ukame wa Somalia watangazwa kimataifa.
Mogadishu, Somalia- 20/07/2011. Umoja wa Mataifa umetangaza ya kuwa Somalia imekua na baa la njaa kimataifa kwa kipindi cha miaka 60 iliyo pita.
Kwa mijibu wa habari kutoka ofisi za umoja wa mataifa zinazo shughulikia chakula zimesema, "Somalia imekuwa na ukame wa kutisha na kuhatarisha maisha ya kila kiumbe hai."
Hata hivyo mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu yamezilaaumu nchi tajiri dunia kwa kutokulipa kipao mbele swala la njaa iliyopo Somali na Afrika ya mashariki kwa ujumla.
Wanchi wa Malawi waandamana.
Lilongwe, Malawi - 20/07/2011. Mamia ya wanchi wa Malwi wamepambana na polisi wa kuzuia ghasia ambao wanadai rais wa nchi hiyo kujitoa madarakani kutokana na kuanguka kwa uchumi na haki za binadamu.
Habari zinasema"raia hao walichoma matairi ya magari na kuharibu baadi ya maeneo."
Msemaji wa polisi, Willie Mwaluka alisema " polisi wapo katika tahadhali kwani hali inaelekea kuwa mbaya na tunajitahidi kutuliza ghasia na kulinda usalama wa raia."
Serikali ya Malawi imekuwa na matatizo ya kiuchumi na Uingereza kusimamisha mchango wake wa kiasi cha £341milion ambazo zimekuwa zikisaidia katika nyanja tofauti nchini humo.
Akiongea katika radio ya taifa, rais wa Malawi Bingu wa Mutharika alisema " wakati nchi zinazo endelea zinasaidiwa kifedha ili kuinua uchumi wake na shirika la fedha, sisi nchi masikini tunaambiwa tupunguze thamani ya fedha zetu hili si jambo jema kwa jumuia ya kimataifa."
Serikali ya Malawi imekuwa na mvutano na shirika la fedha la kimataifa katika swala la kifedha.
Wapinzani wa Gaddafi wakubaliana na Ufaransa
Paris, Ufaransa - 20/07/2011.Serikali ya Ufaransa itangaza ya kuwa kiongozi wa Libya mUammar Gaddafi anaweza kukua nchini Libya ikiwa atakubali kuachia madaraka.
Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Alain Juppe alisema " jumuiya ya nguvu za nje zipo tayari kuruhusu Muammar Gaddafi anendelee kuishi nchini Libya, ikiwa atakubali kuachaia madaraka, na kuwepo kwa amani nchi Libya kupo mikononi mwa Gaddafi na tupo kuwahakikisha ya kuwa Libya ina kuwa huru kutoka mikononi mwa Gaddafi."
Maelezo haya yamekuja baada ya viongozi wa kundi la upinzani linalo pingana na serikali ya Muammar Gaddafi kufanya mazungumzo na serikali ya Ufaransa ambayo inawasaidia kwa hali na mali ili kumuondoa Gaddafi madarakani..
Waziri mkuu wa Uingereza awekwa kiti moto na bunge.
London,Uingereza. 20/07/2011. Waziri mkuu wa Uingereza amekuwa na wakati mgumu kujitete ili kutotikisa uamini wake kwa raia wa Wauingereza na wanachama wa chama chake kutoka na kumwajili mmoja wa aliyekuwa mhariri wa gazeti la News of the world.
David Cameron ambaye amekatisha ziara yake katika bara la Afrika, na kuja kuliongelea swala kumwajili Andy Coulson, kwa kusema " nisingeweza kumwajili Andy kama ningejua hali hii na kwa hilo naweza kuomba radhi kama ikibidi."
Unaishi, kujifunza na kuamini na kwa minajili hiyo ninawajibu kuwajibika ili kutatua swala hili" alisema David Cameron.
Hata hivyo kiongozi wa chama cha upinzani Ed Miliband alisema " David Cameron amefanya makosa katika uamuzi wake."
Kiti moto hicho ambacho alikuwa nacho waziri mkuu wa Uingereza, kimekuja baadaya mmiliki wa gazeti la news of the world ambalo limefutwa, Rupert Mudorch na mtoto wake kumaliza kufanywiwa mahojiano na kamati ya bunge kuhusu gazeti kuhusika na kurekodi simu za watu binafsi kinyume cha sheria.

No comments: