Friday, July 1, 2011

Majina ya washukiwa ya mauaji Rafik Harir yatajwa.

Dominique Strauss-Kahn apata unafuu wa katika kesi yake.
New York, Marekani - 01/07/2011.Mahakama ya jijini New York imemwondolea aliyekuwa mkuu wa shirika la fedha duniani IMF-Intarnational Monitary Fund Dominique Strauss-Kahn, sheria ya kumtaka akae katika nyumba yake bila kutoka wakati kesi yake ikiendelea.
Jaji anayesikiliza kesi hiyo alisisitiza wakati wa kusoma uamuzi huo alisema " kuachiwa huko hakuna maana kesi imefungwa, bali kesi bado inaendelea na haruhusiwi kutoka nje ya nchi."
Hata hivyo hata habari kutoka ofisi ya mwanasheria anayeshughulikia kesi hito zinansema, " uamuzi huo umekuja baadaya ya uchunguzi kuonyesha wasiwasi juu ya kesi yenyewe hasa kutoka kwa mshitaki wa kesi hiyo."
Dominique Strauss-Kahn anakabiliwa na kesi ya kutaka kumbaka mmoja ya wafanyakazi wa hotel aliyokuwa amefikia wiki chache zilizo pita akiwa ziarani kikazi Marekani,
Dominique Strauss-Kahn kama atakutwa na hatia anaweza kuhukumiwa kifungo cha miaka 25 jela.
Rais wa Sudan Omar al bashir ziarani nchini China.
Beijing, China - 01/07/2011. Serikali ya China na serikali ya Sudani zimakubaliana kushirikiana kwa ukaribu zaidi katika sekta ya kiuchumi kufuatia ziara ya rais wa Sudan Omar al- Bashir.
Rasi wa China Hu Jintao ambaye alikuwa mwenyeji wa rais wa Sudan Omar al-Bashir alisema " nifuraha kumkaribisha rais wa Sudan na hii inaonyesha kukua kwa urafiki kati ya nchi hizi mbili China na Sudan na kutaongeza kubadilishana maarifa katika kukuza uchumi kati ya nchi hizi."
Rais Omar al Bashir, ambaye alifunguliwa mashitaka na mahakama ya inayo tetea haki za binadamu, atazungumzia pia hali halisi ya bara la Afrika na mgawanyo wa Sudan unaotarajiwa kutokea July 9.
China imekuwa nchi ambayo inashirikiana kiukaribu na Sudani katika sekta ya kibiashara hasa kwenye uzalishaji wa mafuta.
Majina ya washukiwa ya mauaji Rafik Harir yatajwa.
Beirut. Lebanon-01/07/2011. Waziri wa mambo ya ndani wa Lebabon amethibitisha rasmi majina ya watu wanao shukiwa katika mauaji ya aliyekuwa wazairi mkuu wa Lebanon Rafik Harir na watu wengi 22 mwaka 2005.
Waziri Marwan Charbel alisema ya kuwa , "mwanasheria mkuu wa Lebanon, ametoa kibali cha kukamatwa kwa washikiwa ambao ni Mustafa Bedreddine, Salaim Ayyash amabye anaulaia wa Marekani, Assad Subra na Hussein Anaissi."
Kwa mujibu wa habari zilizo patina zinasema washutumiwa hao hawajulikani wapo wapi na hivyo kesi dihi yao itakuwa wazi mpka hao watakapo kamatwa.
Hata hivyo kundi Hezbollah limekanusha madai hayo na kiongozi wakundi hilo amedaia yakuwa yoyote atakaye karibu "kuwakamata watu hao atakata mikono yao."
Nayo serikali ya Marekani inefurahishwa na kitendo hicho cha kujulikana kwa wahusika wa mauaji ya aliye kuwa waziri mkuu wa Lebanon Rafik Hariri na kusisi tiza ya kuwa haki lazima itendeke.

No comments: