Mahakama ya Uingereza yaruhusu kesi ya rais wa Kenya kuendea.
Jaji katika mahakama hiyo Richard McCombe ambaye alitoa uamizi huo alisema " Washitaki wanaweza kuendelea na kesi hii, kwani ushaidi wa kisheria upo kwa serikali ya Uingereza kujibu mashitaka haya."
Katika kesi hiyo, serikali ya Uingereza imekuwa ikijitaihidi kupinga kuendelea na kesi hiyo, kwa madai yakuwa hilo ni" jukumu la serikali ya Kenya."
Wawakilishi katika kufungua kesi hiyo Ndiku Mutwiwa Mutua, Paulo Muoko Nzili, Mbugua Wa Nyingi na Jane Muthoni Mara ambao wapo na umri kati ya miaka 70 na 80, wanadai ya kuwa serikali ya kikoloni ya Uingereza iliwatesa na kuwapiga na baadhi ya jamaa zao walipoteza maisha kutokana na mateso hayo.
Kesi hiyo inatarajiwa kuanza mapema mwaka 2012.
No comments:
Post a Comment