Sunday, July 31, 2011

Umoja wa Afrika watoa tahadhali za mashambulizi zidi ya Al-Shabab.

Umoja wa Afrika watoa tahadhali za mashambulizi zidi ya Al-Shabab.
Mogadishu,
Somalia - 31/07/2011. Kamati ya usalama ya umoja wa Afrika umetangaza ya kuwa kundi la Al-Shabab linalo pingana na serikali ya Somalia lina panga kufanya mashambulizi wakati wa mwezi mtukufu wa mwezi wa Ramadhani.
Habari kutoka kamati hiyo zinasema " kundi la Al-Shabab limepanga kufanya mashambulizi wakati wa mwezi wa Ramadhani baada ya kupata siriha kutoka kwa kundi washiriki lililopo nchini Yameni."
Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Somalia vimekuwa vikileta matatizo kwa wanchi wa Somalia na hata nchi ambazo zimepakana na nchi hiyo.
Hata hivyo serikali ya Somalia imekuwa ikipambana na kundi hilo ambalo lina sababisha kuwepo kwa ugumu kwa mashirika ya kimataifa yanayo toa misaada ya vyakula nchini Somali kushindwa kusambaza chakula katika maeneo ambayo yamekumbwa na ukame nchini humo.

No comments: