Wednesday, July 27, 2011

Serikali ya Uingereza yaitambua rasmi baraza la mpito la waasi nchini Libya.

Serikali ya Uingereza yaitambua rasmi baraza la mpito la waasi nchini Libya.
London, Uingereza -27/07/2011. Serikali ya Uingereza imefunga ofisi zote za ubalozi wa serikali ya Libya na kuwafukuza wafanyakazi wote ambao wanawakilisha serikali ya Muammar Gaddafi.
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uingereza William Hague aliyasema hayo wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kwa kusema " kuanzia sasa hatuta itambua serikali ya Muammar Gaddafi na uhusiano uliopo wa kidiplomasia na serikali yake tumeufuta."
William Hague aliongezea kwa kusema " tunalitambua rasmi kundi la Walibya wanaoongoza serikali ya mpito kama wawakilishi wa wa Walibya na tutashirikiano nao kikamilifu."
Kufuatia kuvunjika uhusiano wa kidiplomasia serikali ya Uingereza na ya Muammar Gaddafi, serikali ya Uingereza itazifilisi mali zote za serikali ya Libya na kutumika katika kulisaidia kundi linalo pingana na serikali ya Gaddafi.
Wakati huo huo, serikali ya Libya imesema haitafanya mazungumzo yoyote mpaka hapo NATO itakaposimamisha mashambuliz yake nchini humo.
Rais wa zamani wa Misri agoma kula.
Kairo, Misri - 27/07/2011. Aliyekuwa rais wa Misri , amekuwa na matatizo ya kiafya na anakataa kula, wakati kesi zidi yake ikiwa inatayarishwa ili kujibu mashitaka ya kutoa ruhusa kwa polisi kuwauwa na kuwajeruhi waandamanaji waliokuwa kipinga serikali yake mapema mwanzoni mwa mwaka huu.
Kwa mujibu wa habari zinasema " Hosni Mubara anakunywa maji na mwili wake umeanza kukonda na uzito kupungua.
Hosni Mubaraka ambaye ameitawala Misri kwa muda wa miaka 29 kabla ya kutolewa madarakani kwa nguvu za maandamano ya wananchi yaliyo tokea mapema mwaka huu ambapo baadhi ya watu walipoteza maiasha wengine kuumia na maafafa makubwa ya kijamii kutokea.
NATO yaingia kutatua mzozo kati ya Wakosovo na Waserbia.
Brussels,
Ubeligiji - 27/07/2011. Jeshi la nchi za magharibi la NATO limeamua kuingilia kati kutatua mgogoro uliotokea wakugombania mpaka kati ya Wakosovo na Waserbia.
Uamuzi huo wa NATO umekuja baada ya serikali ya Wakosovo kuwekea vikwazo bidhaa zote za Waserbia kupitia nchi humo jambo ambalo limesababisha serikali ya Serbia kutokubaliana nalo.
Jumuiya ya Ulaya imelaani kitendo hicho na kuzitaka pande zote kukaa kwenye meza ya mazungumzo na kulimaliza tatizo hilo mara moja.

No comments: