Sunday, July 3, 2011

Thailand yapata waziri mkuu mpya mwanamke kwa mara ya kwanza.

Thailand yapata waziri mkuu mpya mwanamke kwa mara ya kwanza.
Bangkok, Thailand- 03/07/2011. Waziri mkuu wa Thailand amempongeza mpinzani wake bi Yingluck Shinawatra ambaye ni kiongozi wa chama cha Pheu Thai Party kwa kushinda kura nyingi katika uchaguzi uliyofanyika nchini humo.
Waziri mkuu Abhisit Vejjajiva akitoa pongezi zake alisema " napenda kumpongeza kiongozi wa Pheu Thai Party na nawatakia mafanikio mema katika kuunda serikali mpya na nitampa ushirikiano mkubwa kwani amekuwa kiongozi wa kwanza mwanamke kushika kiti hicho na naimani ataleta ushirikiano mkubwa."
Akiongea baada ya huku matokeo hayo bi Yingluck Shinawatra alisema " swala kubwa ni kuinua uchumi wanchi na kunakazi kubwa ambayo inatukabili wana Thailand na kwa ushirikiano tutafanikiwa."
Bi Yingluck Shinawatra, ambaye ni dada ya aliyekuwa waziri mkuu wa zamani Thaksin Shinawatraaliye ondolewa madarakani mwaka 2006.
Umoja wa Afrika wapinga amri kukamatwa kwa Muammar Gaddaf
Moscow,
Urusi- 03/07/2011. Rais wa Afriak ya Kusini yupo nchini Urusi katika ziara rasmi ili kujadili na kufanya mazungumzo na viongozi wa serikali ya Urusi na kundi linalo shughulikia swala la kuleta amani nchi Libya.
Rais Jacob Zuma, ambaye atawakilisha Umoja wa nchi za Afrika, anatarajiwa kuelezea msimamo wa umoja huo na maamuzi yaliyo fikiwa wakati wa kikao kilicho amalizika hivi karibuni nchini Ekwetaria Guinea.
Hata hivyo kikao hicho hakikubali na kupinga swala la mahakama ya kimataifa ya Hague iliyopo nchi Uhollanzi kwa kutoa amri ya kukamatwa kwa kiongozi wa Libya Muammar Gaddaf kutoka na kudai mahakama hiyo imekuwa "inaaangali makosa yanayo fanyika katika bara la Afrika na kufumbia macho yale yanayo fanywa na nchi za Ulaya Magharibi hasa huko Iraq, Pakistan na Afghanistan na kudai yakuwa Mureno Ocampo analeta mzahaa katika kutimiza na kuangalia haki" alisema Jean Ping ambaye ni mwenyekiti wa umoja huo wa Afrika.

No comments: