Friday, July 29, 2011

Rubani alaumiwa kwa kusababisha ajali ndege

Rubani alaumiwa kwa kusababisha ajali ndege.
Paris, Ufaransa - 29/07/2011.Rubani aliyekuwa akirusha ndege ya shirika la Ufaransa amelaumiwa kwa kusababisha kuanguka kwa ndege iliyopoteza maisha ya watu 228.
Ndege hiyo ambayo ilianguka wakati ilipokuwa ikifanya safari zake za kaiwada kueleka Ufaransa iliaangu kutoka umbali wa mita 40,000 na kutumbukia katika bahari ya Atlantiki mwaka 2009.
Ripoti ilitolewa baada ya kufanyika kwa uchunguzi na BEA inasema " rubani hakuwa amepata mafunzo mazuri ya kurusha ndege hasa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Kuafuatia ripoti hiyo, shirika la ndege la Ufaransa limehaidi kuongeza mafunzo zaidi ya rubani wake ili kuepuka ajali kama hiyo kutokea tena.
Kiiongozi wa kundi la kijeshi la upinzani nchini Libya auwawa.
Benghazi,
Libya - 29/07/2011. Mkuu wa majeshi ya upinzani yanayo mpinga Muammar Gaddafi ameuwawa kwa kupigwa risasi yeye pamoja wasaidizi wake wawili.
Abdel Fattah Younes, ambaye alikuwa mmoja wa wanajeshi waliongoza mapinduzi ambayo yalimweka madarakani Muammar Maddafi 1969, na baadaye kuongoza kama waziri wa mambo ndani hadi hapo alipo jitoa kutoka kwenye serikali ya Muamar Gaddafi na kujiunga na kundi linalo mpinga lenye makao yake makuu Benghazi.
Hata hivyo kifo chake bado kinaleta utata na huenda kikaleta mvutano ndani ya kundi hilo la upinzani.

No comments: