Thursday, July 28, 2011

Muungano wa mashoga watambulika na umoja wa mataifa.

Serikali ya Eritria yakabiliwa na shutuma.
Addis Abeba, Ethiopia-28/07/2011. Serikali ya Eritria imeshutumiwa kwa kutaka kushambualia kikao cha viongozi wakuu wa Afrika kilicho fanyika mapema mwanzoni mwa mwaka huu.
Kwa mujibu wa habari hizo zinasema, " serikali ya Eritria kwa kushirikiana na vikundi vya kigaidi walipanga kuulipua mkutano huo pamoja na sehemu muhimu za jiji la Adis Abeba."
Hata hivyo serikali ya Eritria ilikataa na kusema "haina ushirikiano wowote na makundi ya kigaidi na kudai ya kuwa hiyo ni mbinu za kutaka kuichafua serikali Eritria ," kwani serikali ya Ethiopia ndiyo iliyo ahidi kwa kupitaia waziri wake mkuu ya kuwa itavisadia vikundi vinavyo pingana na serikali ya Eritria."Habari kutoka ofisi ya mambo ya nje ya Erirtia zilisisitiza.
Muungano wa mashoga watambulika na umoja wa mataifa.
New York,
Marekani- 28/07/2011. Umoja wa mataifa umetangaza kutambu muungano wawakilisha mashoga na wale wote ambao wanapendelea kufanya mapenzi kwa watu wa jinsia moja.
Habari kutoka shirika la kutetea haki za binadamu limesema " uamuzi huo wa umoja wa mataifa ni mzuri kwani unaonyesha ni jinsi gani jumuia ya kimataifa inaamini binadamu wote wanaihitaji kupewa haki sawa."
Uamuzi huo wa kutambulika kimataifa kwa muungano wa wawakilishi wa mashoga umekuja wakati bado nchi nyingi hasa Afrika hazitambui haki za mashoga hao.

2 comments:

nael said...

wow
from indonesia

Anonymous said...

Utandawazi huo..tutakoma Tsunami zitazotuhangamiza