Friday, July 15, 2011

Kenya yakubali kufungua kambi nyingine ya wakimbizi.

Serikali ya Muammar Gaddafi bado kitendawili kwa NATO na washiriki wake.
Istambul, Uturuki - 15/07/2011. Serikali ya Amerika imejiunga na nchi nyingine kulitambua kundi la wapinzani wanao pingana na serikali ya Libya inayo ongozwa na Muammar Gaddafi katika mkutano uliofanyika nchini Uturuki jijini Istambul.
Katika mkutano huo ambao umewakutanisha viongozi wa nchi mbalimbali umetamka ya kuwa serikali ya Muammar Gaddafi na watu wake wakaribu wanaotawala hawatambuliki na niwakati wake kuachia madaraka kwa wanchi wa Libya.
Uingereza nchi ambayo ipo mstari wambele katika jitihada za kumngoa madarakani Muammar Gaddafi, imeatangaza kuongeaza misaada ya kijeshi katika jeshi la NATO linalo fanya mashambulizi nchini Libya kwa muda wa miezi minne hadi sasa.
Msemaji wa serikali ya Libya inayo ongozwa na Muammar Gaddaf amekanusha kauli hiyo ya mkutano wa Istambuli kwa kusema " usemi huo wa mkutano wa Uturuki nchini Istambuli hatuutambui na tutapigana hadi kufa kwa kulinda mafuta yetu zidi ya jeshi la NATO, tuta ua tupo tayari kufa kwa mafuta yetu."
Kwa mujibu wa habari kutoka kwenye mkutano huo zinasema " lengo la mkutano huo ni kuangalia kiundani nakutathmini ni kwa jinsi gani Libya itakuwa mara baada ya kuondoka kwa Muammar Gaddaf na serikali yake na vilevile kupanga mikakati mipya ya kumngoa Muammar Gaddaf madarakani.
Bunge la Itali lakubali mbano wa matumizi.
Rome, Italy - 15/07/2011. Bunge nchi Italy limepiga kura nakupitisha mbano wa matumizi na umakini katika kodi za mapato kwa kipindi cha miaka mitatu.
Mbano huo utakao kuwa wa kiasi cha dola za Kimarekani 67 billioni ulipita kwa kura 314 zidi ya zile zilizo pinga 280.
Kwa mujibu wa habari toka serikalini zinasema " serikali imeamua kufanya hivyo ili kulinda uchumi wa nchi hiyo na kufikia malengo yake ifikapo 2014."
Serikali ya Itali imefuata mlolongo wa nchi wanachama wa jumuiya ya Ulaya ambazo ziliamua kuchukua hatua kama hiyo ili kunusuru kuporomoka kwa uchumi wa nchi zao.
Ushindi huo wa kura katika bunge kumezidi kumpa uzima wa kisiasa waziri mkuu wa Italli Silvio Berlusconi ambaye anakumbwa na misukosuko katika uongozi wake hasa kutoka upande wa wapinzani wa serikali yake.
Kenya yakubali kufungua kambi nyingine ya wakimbizi.
Nairobi, Kenya - 15/07/2011. Serikali ya Kenya imekubali kufungua kambi ya ukimbizi iliyopo mpakani kwenye eneo la Ifo II Dabaab, kwa ajili kuwapokea wanchi wa Somalia ambao wanakimbia ukame ulioikumba nchi hiyo na hali ya usalama wa maisha yao kuwa mashakani kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyo chukua zaidi ya miaka 15.
Waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga, alikubali kufunguliwa kwa kambi hiyo mara baada ya kutembelea kambi moja ambayo imewapokea wakimbizi wapatao 100,00o kutoka Somalia.
Raila Odinga, alisema, " ingawaje tunafikilia na kujali usalama wa raia Kenya, lakini hatuwezi kuacha ndugu zetu wateseke, na niwajibu wetu kutoa misaada wa hali na mali."
Msemaji wa shirika la kuhudumia wakimbizi duniani, Fafa Attidzah alisema " tunafuraha na kuishukuru serikali ya Kenya kwa kukubali kufungua kambi nyingine ambayo itatuwezesha kuwapokea wananchi wa Somalia na kuwapa huduma za kibinadamu."
Kambi hiyo ya Ifo II iliyopo Dabaab inatarajiwa kupokea zaidi ya wakimbizi 300000.

No comments: