Saturday, July 23, 2011

Wanorway wapatwa mistuko na mauaji ya mabomu na ya risasi.

Wanorway wapatwa mistuko na mauaji ya mabomu na ya risasi.
Aslo, Norway-23/07/2011. Wanachi wa Norway bado wapo katika mshituko mkubwa baada ya milipuko ya mabomu na mtu mmoja aliyeva nguo za polisi kuwaua watu waliokuwepo katika kisiwa cha Utoya nchi humo.
Mauaji hao ambayo yametokea kwa kufuatana, mabomu yalisababisha mauaji ya watu 7 na katika kisiwa cha Utoya watu zaidi ya 84 waliuwawa na wengine kujeruhiwa vibaya na mtu huyo aliyevaaa kama askari polisi wakati wakiudhulia mkutano wa umoja wa vijana wa chama cha Labour.
Polisi wamemkamata mtu mmoja raia wa Norway Anders Berring Breivik 32 kwa mahijiano zaidi kufuatia matukio hao.
Viongozi wa serikali tofauti duniani wametuma salamu za rambirambi kwa serikali ya Norway kufuatia mauaji hayo ya kutisha yaliyo wakuta wanchi wa Norway.
Muammar Gaddafi bado mthiani kwa wapinzani na NATO.
Tripoli, Libya -23/07/2011. Milipuko mikubwa ya mabomu imesikika katika jiji la Tripoli huku mamia wakiakiandamana kumuunga mkono Muammar Gaddafi.
Mamia ya waandamanaji walikusanyika mbele ya bendera kubwa yanye picha ya kiongozi huo na kusema wanamuunga mkono mpaka mwisho.
Kwa mujibu wa habari kutoka serikali ya Libya zinasema " mabomu hayo yalishambulia maeno ya hotel za kitalii."
Wakati huo, kundi la upinzani linalo mpinga Muammar Gaddafi linamsema " tumefanikiwa kumkamata mmoja wa viongozi wa kijeshi generali Abdul Nabi Zayed ambaye ni mafaniko makubwa kwetu kwani alikuwa mmoja ya viongozi ambao walikuwa nawapanga mbinu za kimashambulizi zidi yetu, na vilevile tunakaribia kuukamata mji wa Zliten na pia baadhi ya wapiganaji wetu wameweza kuingia ndani ya jiji la Tripol."
Mapigano yanayo endela kati ya wapinzani wa Gaddafi na serikali yake yamesha chukua zaidi ya miezi mitatu na kusababisha maafa makubwa kijamii na kimazingira.
Mashambulizi ya jeshi la NATO yamekuwa yakifanyika ili kumlazimisha Muammar Gaddafi aachie madaraka.
Wapalestina wahaidi kudai utaifa wao Septemba mwaka huu.
Istambul. Uturuki - 23/07/2011. Rais wa serikali ya Wapalestina ameliambia baraza la washiriki walioshirikia katika mkutano uliofanyika nchini Uturuki ya kuwa serikali yake imeamua na kuongoza nia ya Wapalestina kutaka kutambulika kama taifa huru ifikapo mwezi Septemba.
Rais Mahmoud Abbas alisema " tunaenda umoja wa mataifa kudai haki ya kuwa taifa huru baada ya serikali ya Izrael kutulazimisha kufanya hivyo kwa kuendelea na kitendo cha kujenga makazi katika eneo letu."
Na tumekutana ili kuandaa mikakati kamili ya kudai haki zetu katika baraza kuu la umoja wa mataifa." Alisema raia Abbas.
Mgogoro wa Wapalestina na Waizrael ni wa muda mrefu, ambao bado unaleta kichwa kuuma kwa jumuia ya kimataifa, na hasa inapofikia makubaliano ya mpaka kuwa wapi kufuatia makubaliano ya mwaka 1967.

No comments: