Sunday, July 31, 2011

Rwanda nchi ya kwanza duniani kuwa na wabunge wengi wanawake.

Rwanda nchi ya kwanza duniani kuwa na wabunge wengi wanawake.
Kigali, Rwanda - 31/07/2011. Nchi ya Rwanda imekuwa nchi ya kwanza duniani kwa kuwa na wabunge wanawake katika bunge la nchi hiyo.
Bunge hili lenye ambalo lina viti 80 na 45 kati ya viti hivyo vinashikiliwa na wanawake.
Rwanda nchi ambayo mwaka 1994 ilikumbwa na mauaji wa kikabila, imekuwa ikichukuliwa kama mfano bora kwa kujaribu kuwapa wanawake nafasi sawa na wamume katika kujenga uchumi wa nchi hiyo.
Viongozi wa zamani wa Tanzania waonya mvurugano bungeni.
Dar es Salaam, Tanzania - 31/07/2011. Viongozi wastaafu wa serikali ya Tanzania wamelilaumu bunge lilipo katika kipindi hiki ya kuwa halifanyi kazi inayo takiwa kama bunge.
Viongozi hao Joseph .S. Warioba na Salim .A. Salim, ambao walishawahi kuwa mawaziri wakuu wakati wa utalwala wa aliyekuwa rais wa kwanza wa Tanzania hayati Mwalimu Julias K Nyerere kwa pamoja walisema, " bunge la sasa hivi lililopo bungeni halifanyi kazi yake na limekosa mwelekeo wa kutetea wananchi na kupanga malengo ya kujenga na kuinua uchumi wa nchi, lakini matokeo yake wabunge wote wanaaangalia maslahi yao ya kisiasa na vyama vyao. Na ule utaifa, uzalendo wa kupenda, kulinda na kujenga nchi umekwisha kwa viongozi wetu walipo madarakani na wanchi kukusa imani.
Viongozi hao pia walitaka tabia hiyo ikome, kwani kuwepo kwa mfumo wa vyama vingi siyo mwanzo wa kureta fujo na kuondoa amani, bali watumie mfumo huu kuuimarisha umoja na kujenga nchi japo wanatofautiana kiitikadi, kwa kuzingatia nchi hiyo ipo katika hali isiyo nzuri kwa kukosa umeme na kupanda kwa hali ya maisha.
Na walisitiza kuwepo na mwamko mpya wa uzalendo na utaifa ambao rais wa kwanza wa nchi hiyo hayati Julias K Nyererer aliujengea misingi bora.
Maonyo ya viongozi hao yamekuja baada ya bunge la nchi hiyo kuwa na vurugu kati ya wabunge wa vyama vya upinzani na wabunge wa chama tawala katika miswaaada mbalimbali inayoletwa bungeni humo.
Namibia yagundua kuwepo na mafuta nchini humo.
Windhook,
Namibia - 31/07/2011. Serikali ya Namibia imetangaza hivi karibuni ya kuwa imegundua kuwepo kwa mafuta kwenye eneo lililopo Kusini mwa pwani ya nchi hiyo.
Waziri wa nishati na madini Isak Katali alisema " kugunduliwa kwa mafuta hayo ambayo yatakapo anza kuchimbwa yatasaidia kuinua uchumi wa Namibia na maisha ya watu wote kwa ujumla."
Kunaaaminika ya kuwa kuna zaidi ya magalloni billioni 13 ambayo yataifanya Namibia kuwa nchi ya tano katika uchimbaji wa mafuta katika bara la Afrika baada ya zile za Libya, Nigeria, Algeria na Angola.

2 comments:

Anonymous said...

Tatizo kuu ni Uwoga Mkuu wakati wa nchi ilipokuwa chini ya chama kimoja na Bunge kutumika kama chombo cha kupitisha hoja bila kuhuliza wala kupinga..sasa hivi angalau kidogo maana halisi ya bunge tunaanza kuliona..Bravo Chadema.NCCR,nk

Anonymous said...

Bunge sio Msikiti,Hekalu au Kanisa,ni sehemu ambayo kero,kilio na matakwa ya wananchi chini ya wawakilishi wao wanapofikisha hoja zao..jee kweli kwa stile ya ukondoo ukondoo dhidi ya watawala bunge husika kweli litafanikiwa kuwakilisha kilio cha wananchi dhidi..? Tutazame mabunge ya wenzentu kwanza hata hivyo viti vya bungeni ni tofauti na makochi yetu bungeni..vikao vyenyewe huku hata hao wawakilisha mahudhulio yao ni hafifu..