Sunday, July 24, 2011

Mshitakiwa wa mauaji ya Norway atubu kwa madai.

Mshitakiwa wa mauaji ya Norway atubu kwa madai.
Oslo,
Norway -24/07/2011. Mshitakiwa ambaye anashikiliwa na polisi kwa makosa ya kuhusika na mauaji kwa kuwapiga sirasi zaidi ya watu 90 na wengine kupoteza maisha kutokana na tukio hilo,anataraijwa kufikishwa mahakani ili kujibu mashitaka zidi yake.
Anders Breivik, ambaye amekubali kuhusika na mauaji hayo ametoa maelezo kupitia mwanasheria wake kwa kusema " nimeamua kufanya jambo hili ili kuleta mageuzi katika jamii ya nzima ya wanachi wa Norway."
Mshitakiwa huo ambaye inaaminika ni mkristu mwenye imani kali na ni mwanchama wa kundi la watu wenye itikadi kali ambao wanapinga kuwepo kwa wageni nchini humo na hasa wale ambao ni waumini wa dini ya Kislaamu na pia inasemekana alisema alikuwa amepanga kufanya kitendo hicho cha mauaji kwa toka siku za nyumu.
Wakati huo huo maelfu ya Wanorway wafanya misa na ibada za maombelezi kuwaombea wale wote walifariki kutokana na mauaji ya mlipuko wa mabomu na mauaji ya kupigwarisasi yaliyo tokea nchini humo.

1 comment:

Anonymous said...

Lakini cha kusikitisha huo mkusanyiko wa hao vijana ni wale ambao imani na mtazamo ni wa Philosoph na idea za NAZI-Hitler..ambao ni hatari sana kwa uwepo wao hapa Duniani..hilo naona vyombo vya habari vinaficha..