Friday, July 22, 2011

Sitaongea na wapinzani hadi siku ya kiama asema Muammar Gaddafi.

Mtuhumiwa wa vita akamatwa na kuwasilishwa Uhollanzi.
Hague, Uhollanzi- 22/07/2011. Kiongozi wa kivita vilivyotokea Kroatia kati ya 1991-199 amewasilishwa nchini Uhollanzi ili kujibu mashitaka ambayo yanamkabili kuhusika katika vita na mauaji.
Goran Hadzic, ambaye atakuwa mtuhumiwa wa mwisho katika kesi hii alikamatwa karibu na misitu Fruska Gorakilomota 65 kaskazini mwa jiji la Belgrade.
Kabla ya kuondoka Goran Hadzic aliruhusiwa kuonana na ndugu na jamaa zake akiwepo mama yake mzazi.
Kukamatwa huko kwa Goran Hadzic kunatarajiwa kurahisisha kwa Belgredi kusukuma mpango wa nchi hiyo kujiunga na umoja wa Ulaya.
Umoja wa mataifa kichwa kuuma zidi ya Morokko na Sahara Magharibi
New York - Marekani 22/07/2011. Kikao kilicho itishwa na umoja wa mataifa ili kujadili hali ya maelewano kati ya Morokko na Sahara ya Magharibi kimekwisha bila kufikia muafaka.
Msimamizi wa mkutano huo, ambao ulifanyika jijini New York Christopher Ross alisema " kila upande bado unashikilia msimamo wake jambo ambalo limefanya majadiliano kuwa magumu."
"Hata hivyo pande zote mbili zimekubaliana kushiriki katika mazungumzo yayote ya hapo baadaye."
Mgogoro wa Morokko na Sahara ya Magharibi umekuwa wa muda mrefu, jaambo ambalo umoja wa mataifa bado inalitafuatia ufumbuzi.
Sitaongea na wapinzani hadi siku ya kiama asema Muammar Gaddafi.
Tripoli, Libya - 22/07/2011. Kiongozi wa Libya amewahutubia wanachi na wale wote wanaomuunga mkono ya kuwa hatafanya mazungumzo na kundi la wapinzani wa serikali yake hatasiku moja mpaka siku ya kiama.
Muammar Gaddafi ambaye amatawala Libya kuwa muda mrefu alisema " siwezi kufanya mazungumzo na kundi lolote linalao pingana na serikali yetu na haitawahi kutokea hadi siku ya kiama."
Wakisikiliza ujumbe wa kiongozi wao Muammar Gaddafi,mamia ya wakazi wa Tripoli ambao walikusanyika kumsikiliza huku wakishangilia kwa kupeperusha bendera za kijani na huku wakiwa wamebeba mabango na maandishi kwenye nguo zao zilioandika kumuunga mkoni Muammar Gaddafi, licha ya mashambulizi yanayo endelea na jeshi la NOTO nchini humo.
Kwa mujibu wa habari kutoka kwa wataalamu wa maswala ya siasa za Libya wamasema " yaelekea hotuna za Muammar Gaddafi zinaleta ugumu kwa kundo la wapinzani kila siku."

No comments: