Thursday, July 14, 2011

Serikali ya Sudani ya Kusini inawakati mguu kukuza sekta ya afya.

Serikali ya Sudani ya Kusini inawakati mguu kukuza sekta ya afya.
Juba,Sudan ya Kusini - 14/07/2011. Wananchi wa Sudani ya Kusini ambao wanasherekea kuzaliwa upya kama taifa huru tangu tarehe 09/ Julai/ 2011 na kujulikana kamataifa kama nchi huru na umoja wa mataifa kuitambua nchi hiyo na kuipa uanachama namba 193 katika umoja mataifa, imegundulika ya kuwa serikali itakuwa na wakati mgumu wakujenga muundo mbinu wa kiafya na nyanja zake.
Habari zilizo patikana zinasema, "miundo mbinu ya kiafya katika hospitali zilizopo nchini humo zinaupungufu mkubwa wa nyenzo za kufanyia kazi na hii nikatika maeneo yote hadi kwenye kambi za jeshi."
"Wafanyakazi wa hospitali hizo ambao wanapokea zaidi ya wagonjwa 200 kwa siku, wana fanya kazi katika mazingira mangumu." Habari zimesema.
Sudani ya Kusini ni nchi ambayo imeundwa baada ya wanchi wa nchi hiyo kupiga kura ya maoni na kuunga mkono kugawanyika kwa nchi ya Sudan.
Serikali ya India ya wasaka waliohusika na milipuko jijini Mumbai.
Mumbai, India - 14/07/2011. Polisi nchini India bado wanaendelea kufanya uchunguzi ili kujua ni kundi gani ambalo limehusika katika mashambulizi ya mabomu yaliyo tokea jiji humo.
Waziri wa mambo ya ndani Palaniappan Chidambaram alisema " milipuko hiyo ambayo imetokea inaashiria ya kuwa ilikuwa ni mpango wa magaidi ili kutishia wanchi wa India ambao hawata tishika kamwe."
Milipuko hiyo ambayo imetokea jijini Mumbai imekuwa ikidhaniwa yakuwa kuna makundi ambayo yanahusika, japo mpaka sasa hakuna kundi ambalo limekubali au kutangaza kuhusika na milipuko hiyo ambayo imeleta maafa makubwa kupoteza maisha ya watu zaidi ya 21 na wengine kujeruhiwa vibaya.
Mashambulizi hayo ni ya pili tangu yale yaliyo tokea mwaka 2008, ambapo kundi la kigaidi kutoka Pakistan Lashkra-e- Taiba lililaumiwa kwa kuhusika namilipuko hiyo na kuzika nchi ya India na Pakistani katika wakati mgumu wa kidipromasia
Dawa ya ukimwi yaleta matumaini mazuri.
New
York, Marekani - 14.07/2011. Shirika linalo shughulikia maswala ya afya la umoja wa mataifa WHO limetoa habari yakuwa dawa zinazo tumiwa na ugonjwa wa ukimwi zinapunguaza kwa kiasi fulani maambukizo ya ugonjwa huo.
Shirika la afya limetoa habari hizo kufuatia uchunguzi uliofanyika nchini Kenya, Uganda na Botswana na kusema " 62% zinaonyesha watu waliotumia dawa hizo walipunguza kwa kiasi maambukizi ya ugonjwa ukimwi kwa wapenzi wao."
Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Margaret Chan alisema " WHO inaendelea kudumisha kazi yake ya kutoa dawa za ukimwi ili kupunguza ugonjwa huo hasa katika nchi hambazo hazina uwezo kiuchumi."
Wachunguzi wa mambo ya kiafya wamelifurahi matokeo hayo ya matumizi ya dawa hizo.

No comments: