Maandamano yafanya rais wa Misri kuvunja serikali.

Maandamano yafanya rais wa Misri kuvunja serikali.

Posted by
Kibatala
at
Saturday, January 29, 2011
1 comments
Nelson Mandela aruhusiwa kutoka hospital.
Johannesburg, Afrika ya Kusin - 28/01/2011. Aliyekuwa rais wa kwanza baada ya kuanguka kwa utawala wa kibaguzi wa makaburu ameruhusi kutoka hospital Mill Park ambako alikuwa amekwenda kwa matibabu.
Nelson Mandela mwenye umri wa miaka 92 alikuwa hospitalini kwa matibabu baada ya kutojisikia vizuri kiafya.
Makamu wa rais Kgalema Motlanthe aisema " Mandela ana nafuu na alikuwa anataniana nasi na tuzidi kumwombea afya yake iwe nzuri."
Picha hapo juu anaonekana Winnie Mandela akitokea hospital kumwangalia mumewe Nelson Mandela ambaye alikuwa amelazwa hospital.
Serikali ya Misri ipo njia panda.
Kairo, Misri 28/01/2011.Maelfu ya wananchi nchini Misri wameandamana kupinga serikali iliyopo madarakani na huku polisi wakipambana na waandamaji kwa kutumia gasi na maji.
Posted by
Kibatala
at
Friday, January 28, 2011
0
comments
Uchumi wa dunia kujadiliwa tena Davos.
Davos,Swiss - 26/01/2011. Viongozi wa serikali, wafanya biashara,,wanasiasa na wanauchumi, wanakutana nchi Uswisi ili kujadili mpangilio mzima wa uchumi dunia. Mkutano huo ambao utachukua siku tano, unatarajiwa kujadili mbinu za kuinua uchumi baada ya mtikiso mkubwa wa uchumi ulio ikumba dunia miaka miwili iliyo pita.
Kwa mujibu wa wachunguzi wa maswala ya kiuchumi wanasema " inabidi katika mkutano huu viongozi, wanasiasa,wafanya biashara na wanauchumi watafute ufumbuzi wa kuinua uchumi na siyo kuweka ahadi ambazo zimekuwa ziki tawaliwa na mzunguko wa siasa na hai halisi ya kiuchumi.
Picha hapo juu ni mji wa Davos, ambao viongozi wa nchi tofauti, wafanya biashara, wanasiasa na wanauchumi wanakutana kujadili hai halisi ya uchumi duniani.
Tunis,Tunisia - 26/01/2011. Polisi wa kimataifa wameombwa kukamata aliye kuwa rais wa Tunisia, mkewe na washiriki wa karibu wa familia yake ili wajibu mashitaka mbele ya mahaakama.
New York, Amerika - 26/01/2011. Umoja a Mataaifa umeombwa kuchangia mbinu mbadala za kupambana na maharamia waliopo katika pwani ya Somalia hadi kufikia pwani za Afrika ya Mashariki na kuanzisha koti maarumu itakayo husika na kesi za kiaaramia.
Posted by
Kibatala
at
Wednesday, January 26, 2011
0
comments
Ukanda wa Magharibi, Palestina - 25/01/2011. Serikali ya Wapalestina imekanusha vikali habari zilizo patikana ya kuwa uongozi huo umeridhia swala Wakimbizi wa Kipalestina.
Posted by
Kibatala
at
Tuesday, January 25, 2011
0
comments
Tony Blair awekwa kiti moto tena
London, Uingereza - 22/01/2011. Aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza wakati wa vita vya Irak na kumtoa madarakani hayati Saadam Hussein ameojiwa kwa mara nyingine tena na tume ya uchunguzi wa mwenendo mzima wa vita vya Irak.
Tony Blair ambaye alikuwa waziri mkuu wa Uingereza, chini ya serikali yake alishirikiana na serikali ya Amerika iliyo kuwa ikiongozwa na rais George Bush na kumn'goa madarakani rais Saadam Hussein wa Irak.
Akiongea mbele ya tume hiyo Tony Blair alisema " nasikitika kwa kwa wale wote waliopoteza maisha au kuathirika kutokana na vita hivi." Na nilimwahidi rais wa Amerika ya kuwa kutakuwa bega kwa bega katika vita hivi kwani niliamini Saadam Hussein alikuwa kiongozi hatri kwa jumuia ya kimataifa."
Uingereza na Amerika kwa kushirikiana na washiriki wengine ziliongoza vita vilivyo vikia kungólewa madarakani kwa rais wa Irak, Saadam Hussein.
Picha hpo juu ni ya aliye kuwa waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair ambaye aalikuwa akijibu maswali kutoka katika tume ya kuchunguza mwenendo mzima wa vita vya Irak.
Paris,Ufaransa - 22/01/2011. Kiongozi wa kundi la Al Qaeda ametishia na kuitaka serikali ya Ufaransa kutoa wanajeshi wake aliopo katika nchi za Kiislaam.
Posted by
Kibatala
at
Saturday, January 22, 2011
0
comments
Odinga, Ouwattara na Gbagbo hakuna maelewano.
Abidjan, Ivory Coast-19/01/2011. Msuruhishi wa mgogoro wa kisiasa nchini Ivory Coast ambaye pia ni waziri mkuu wa Kenya ameondoka nchi humo bila kupata suruhisho la mgogoro huo.
Tunis, Tunisa- 19/01/2011. Rais wa kipindi cha mpito nchini Tunisia ametangaza yakuwa atahakikisha maswala yaliyo leta kutokuelewana na kunyanyasa wanachi hayatarudiwa tena na kutaka wanchi wa Tunisia kufungua ukurasa mpya.
Fouad Mebazaa, akitangaza kupitia TV na vyombo vingine vya taifa na kimataifa alisema, sisi sote kwa pamoja tunaweza kuiongoza na kuijenga nchi yetu na hivyo tufungue ukurasa mpya ili kuijenga nchi yetu ambayo imeyumba kisiasa na kiuchumi."
Hata hivyo bado kunahali ya mvutano wa kisiasa nchini Tunisia huku wanchi wakudai ya kuwa bado serikali hiyo inaviongozi waliokuwa wakati wa utawala wa rais Zine Ben Ali ambaye ameikimbia nchi baada ya wanachi kutaka atoke madarakani.
Nayo serikali ya Swissi imezizuia mali zote za aliyekuwa rais wa Tunisia Zine Ben Ali.
Picha hapo juu anaonekana rais wa mpito wa Tunisia Fouad Mebazaa akishuka kutoka kwenye gari, huku akiwa analindwa vikali na walinzi wake tayari kuelekea ofisini kuanza kazi rasmi ya kuongoza nchi.
Ombi la kukamatwa kwa Tzipi Livni lakataliwa.
Pretoria, Afrika ya Kusini- 19/01/2011. Serikali ya Afrika ya Kusini imekataa ombi la kutaka akamatwe aliyekuwa waziri wa mambo ya nchi za nje wa Izrael ambaye anatarajiwa kufanya ziara nchini humo.
Ombi hilo lilitolewa na Shirika la Uhusiano la Wapalestina, kwa adai ya kuwa aliyekuwa waziri wa mamboya nje wa Izrael Tzipi Livni alihusika katika wakati jeshi la Izrael lilipo shambulia eneo la Gaza mwidho wa mwaka 2008 hadi mwanzoni mwa mwaka 2009.
Mclntosh Polela ambaye ni msemaji wa ofisi ya usalama na makosa ya jinai alisema "tumepata ombi la kutaka kukamatwa kwa aliyekuwa waziri wa mambo ya njee wa Izrael na hatutachukua hatua hiyo na Tzipi Livni hatakamatwa kwani hakuna ushahidi wa kutosha zidi yake."
Picha hapo juu ni ya Bi Tzipi Livni, ambaye alikuwa waziri wa mambo ya njee kati ya miaka ya 2009-9.
Posted by
Kibatala
at
Wednesday, January 19, 2011
0
comments
Posted by
Kibatala
at
Saturday, January 15, 2011
0
comments
Wahaiti wakumbuka siku ya tetemeko la ardhi.
Port au Prince, Haiti - 13/01/2011. Maelfu ya wananchi wa Haiti wamekutana katika jiji la Port au Price kukumbuka siku ambayo tetemeko la ardhi lilitkea na kupoteza maisha ya watu na kuleta maafa makumbwa kwa kila jamii kiuchumi na kiafya.
Tetemeko hilo ambalo lilipoteza maisha ya watu wapatao 316,000 kupoteza maisha yao na wengine kujeruhiwa vibaya.
Kwa mujibu wa mashirika tofauti yanayotoa misaada nchini Haiti yamesema " hadi kufikia sasa hali nchini humo bado siyo ya kulizisha na juhudu zinatakiwa kuongezeka ili kuijenga nchi hiyo na kuinua hali ya misha ya watu wake."
Picha hapo juu ni misaraba ikiwa inawakilisha watu waliopoteza maisha wakati wa tetemeko la ardhi lililo tokea mapema mwaka 2010.
Waamerika waombwa kuungana na kushirikiana.
Tucson, Amerika - 13/01/2011. Rais wa Amerika amewataka Waamerika wote kuungana na kuishi kwa ushirikiano ijapokuwa kunatofauti za kisiasa.
Rais, Baraka Obama aliyasemahayo wakati alipo udhulia siku maalumu ya kuwakumbuka watu walioshambuliwa kwa risasi na kupoteza maisha ya kwenye jimbo la Arizona.
Baraka Obama alisema " mambo mabaya hutokea na nilazima tujitahidi kuwa wavumilivi hasa tukizingatia tumepoteza watu sita kutokana na ukatili uliofanyaka."
Mtu anayehusika na mauaji hayo Jared Lougher 22 anashikiliwa kutokana na kufanya kitendo hicho cha kikatili.
Picha hapo juu wanaonekana rais Baraka Obama akiwa na mke wake Micheel wakishika kwenye ndege kuelekea kuhudhulia siku maalumu ya kuwakumbuka watu waliopoteza maisha wakati wa mashambulizi ya kikatili.
Posted by
Kibatala
at
Thursday, January 13, 2011
1 comments
Kesi ya Julian Assange yaanza kusikilizwa.
Brisbane, Australian - 12/01/2011. Maelfu ya wakazi wa mji wa Brisbane wamehama mji mara baada ya mji mzima kukumbwa na mafuriko ya kihistoria.
Beiruti, Lebannon - 12/01/2011. Serikali ya Lebanon imevunjika baada ya washiriki katika serikali ya muungano Hezbollah kujitoa.
Posted by
Kibatala
at
Wednesday, January 12, 2011
0
comments
Wasudan wapiga kura kuamua muungano wa nchi yao.
Posted by
Kibatala
at
Sunday, January 09, 2011
0
comments
Al shabab walaumiwa kwa kuzuia misaada ya utu.
Mogadishu, Somalia - 07/01/2010. Serikali ya Somalia inalimaumu kundi la Al Shabab kwa kuzuia misaada ya kiutu ambayo inatolewa ja jumuiya ya kimataifa.
Habari kutoka wizara ya mambo ya ndani ya nchi zinasema ' inakuwa vigumu kusambaza misaada ya kiutu kutokana na hali ya kutokuwepo kwa usalama kwa wafanyakazi wanaohusika katika kutoa misaada."
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, Somalia ni moja ya nchi ambayo ilikubwa na hali ya ukame, kiasi cha kuhatarisha hata mifugo.
Picha hapo juu inaonyesha ni kwa kiasi gani hali ya ukame ilivyo hasili maisha ya watu na na wanyama.
Posted by
Kibatala
at
Friday, January 07, 2011
0
comments
Laurent Gbagbo na Alassane Ouattara wakubali kukutana.
Posted by
Kibatala
at
Tuesday, January 04, 2011
0
comments
Brazil wapata rais wa kwanza mwanamke.
Brasilia, Brasil - 02/01/2011. Wananchi wa Brazil wameshuudia kuapishwa kwa rais mpya wa nchi yao, baada ya muda wa rais wa sasa Luiz Lula da Silva kumalizika.
Dilma Rousseff aliapishwa mbele ya watu wapatao 70,000 wakiwemo wageni waalikwa kutoka nchi tofauti duniani.
Rais Dilma aisema " nitajitahidi kulinda na kuendeleza yale yote ambayo rais Luiz Inacio Lula Da Silva aliyo fanya katika kuinua uchumi wa wanchi wa Brazil na kuinua kiwango cha kila mwanchi kiuchumi."
Picha hapo juu anonekana rais wasasa wa Brazil Dilma Rousseff kushoto akiwa na rais aliye mwachia ofisi Luiz Inaci Lula da Silva kwa pamoja wakiwa wamenyanyua mikono mara baada ya kuapishwa kwa Dilma Rousseffe kuwa rais wa kwanza mwanamke.
Urussi yaaanza kuiuzia China mafuta.
Posted by
Kibatala
at
Sunday, January 02, 2011
0
comments
Dunia nzima yashangilia kuanza mwaka 2011.
Posted by
Kibatala
at
Saturday, January 01, 2011
0
comments
Laurent Gbagbo akutana na viongozi wa ECOWAS.
Moscow, Urussi - 28/12/2010. Serikali ya Urussi imezitaka serikali za nchi nyingine kutoingilia mambo yake na nchi hizo zitizame maswala ya nchi zao.
Posted by
Kibatala
at
Tuesday, December 28, 2010
0
comments
Makampuni ya Amerika yafanya biashara za kijamii na Iran.
Seoul, Korea ya Kusini 24/12/2010. Serikali ya Korea ya Kusini inaamini ya kuwa serikali ya Korea ya Kaskazini huenda ikafanya majaribio ya bomu la nyuklia mapema mwakani.
Kutikana na ripoti kutoka wizara ya mabo ya nje ya Korea ya Kusini zinasema "majaribio hayo yatafanywa na Korea ya Kaskazini ikiwa ni njia moja wapo ya kukuza na kuangalia uwezo wa wake wa nguvu za Kinyuklia. Na majaribio hayo yatasababisha hali kuwa ya wasiwasi zaidi kati nchi hizo mbili."
Korea ya Kaskazini ilifanya majaribio tofauti ya kinyuklia mwaka 2006 na 2009 kwa mujibu wa habari zinazoeleweka kimataifa, lakini Korea ya Kaskazini yanyewe haijawai kutamka kuhusu swala hilo.
Picha hapo juu anaonekana mmoja wa mwanajeshi wa Korea ya Kaskazini akiwa katika moja ya vituo vilivyopo mpakani na Korea ya Kusini tayari kwa kazi ya ulinzi huku akiwa ameelekeza bundiki tayari.
ECOWAS uenda ikatumia nguvu nchini Ivory Coast.
Abidjan, Ivory Coast - 24/12/2010. Viongozi wa shirikisho la uchumi wa Afrika ya Magharibi (ECOWAS) wamemtaka rais wa sasa wa nchi hiyo kuachia madaraka mara moja.
Viongozi wa shirikisho la ECOWAS walisema "ikiwa rais Gbagbo hatafanya hivyo basi itabidi nguvu zaidi itumike."
Agizo hilo lilitolewa na viongozi wa ECOWAS lenye nchi wanachama 15 wakati walipo kutana jijini Abuja kujadili hali halisi ya Ivory Coast.
Vurugu za kisiasa nchi Ivory Coast zilizidi mara baada ya matokeo ya uchaguzi wa rais kutangazwa na rais Laurant Gbagbo kudai ya kuwa ameshinda na huku mpinzani wake Alassane Ouattara akidai yeye ndiye aliye shida uchaguzi wa rais.
Picha hapo juu anaonekana rais wa sasa wa Ivory Coast Laurent Gbagbo akiongea wakati wa kampeni zake za uchaguzi wa rias.
Posted by
Kibatala
at
Friday, December 24, 2010
0
comments
India na Urussi kushirikiana kwa ukaribu zaidi.
New Delhi, India - 21/12/2010. Serikali ya India na Urussi zimekubaliana kwa pamoja kushirikiana katika nyanja za kiusalama na kutiliana mikataba ya kibiashara uchumi na sayansi.
Rais wa Urussi Dmirty Medvedev na waziri mkuu wa India Manmohan Singh walikubaliana mikataba hiyo wakati walipo kutana na kuzungumza ili kudumisha uhusiano zaidi.
Ziara hiyo wa rais wa Urussi imekuja baada ya ziara za kufuatana za viongozi wa Uingereza, Amerika, China na Ufaransa kufanya ziarani nchini India ili kudumisha ushirikiano wakaribu.
Picha hapo juu wanaonekana rais wa Urussi Dmirty Medvedev kushoto akipeana mkono na waziri mkuu wa India Manmouhan Singh mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao.
Irak yapata serikali mpya.
Posted by
Kibatala
at
Tuesday, December 21, 2010
0
comments
Baraka Obama atangaza hali halisi ya Afghanistan.
Washington, Amerika 15/12/2010 - Serikali na washiriki wake wanafanya kazi nzuri katika kuijengaAfghanistan na kuwaanda wananchi wa Afghanistan kuijenga nchi yao.
Rais Baraka Obama, alisema "ingawaje hali ni ngumu lakini hii siyo kikwazo kwani, na nashukuru wale wote waliojitolea na kuendelea kujitolea pamoja na wapiganaji wetu ambao wanafanya kazi usiku na mchana ili kuijenga Aghanistan."
Akiongezea rais alisema, "maendeleo yanaonekana na maendeleo haya ndiyo msingi mkubwa wa kuwafanya wananchi wa Afghanistan kuamini yakuwa kazi iliyo fanywa na jumuiya ya kimataifa ilikuwa ni kwa ajili ya wanachi wa Afghanistan."
Baraka Obama, ameongea hayo ili kuwahakikishia wanachi wa Afghanistan ya kuwa Amerika ipo pamoja nao.
Picha hapo juu anaonekana rais Baraka Obama, akiongea na waandishi wa habari ili kuzungumzia hali halisi ya Afghanistan na mipango ya kuisadia nchi hiyo kimaendeleo.
Hatimaye mwanzilishi wa Wiki Leaks akubaliwa dhamana
New Dheli, India - 15/12/2010. Waziri mkuu wa China amefanya ziara nchini India ili kuendeleza uhusiano wa nchi hizo mbili.
Posted by
Kibatala
at
Thursday, December 16, 2010
0
comments
Irak yaondolewa vikwazo na Umoja wa Mataifa.
New York, Amerika - 15/12/2010.Kamati ya usalama ya umoja wa Mataifa imeiondolea vikwaza nchi ya Irak iliyo kuwa imeviweka kwa muda wa zaidi ya miaka 19.
Akiongea katika mjadala wa kutaka kuiondolea vikwazo Irak, makamu wa rais wa Amerika Joe Biden alisema "Irak inahitaji kuwa katika kiwango cha kimataifa kwa kujitegemea yenyewe na demokrasi ndiyo msingi mkubwa ambo utifanya nchi hiyo imeze kuendelea na Wairak wameonyesha uwezo huo. Pia ni muhimu kwa Irak kuwa na uhusiano mzuri na majirani zake kwani bado Wairak wanamthian mkubwa mbeleni."
Katika kikao hicho, kamati ya usalama iliondo vikwazo vyote ilivyoviweka kwa Irak na kupitisha mswada ambao umeiruhusu Irak kuweza kujenga mtambo wa nyuklia kwa matumizi ya kawaida.
Vikwazo kwa Irak viliwekwa mwaka 1991 na umoja wa Mataifa mara baada ya Irak kuivamia Kuwait mwaka 1990 enzi ya utawala wa rais Saddam Huissen ambaye alitolewa madarakani na serikali ya Amerika mwaka 2003 baada ya kushukiwa kuwa na siraha za kuangamiza jamii.
Ghana kuanza kuzalisha mafuta.
Akrah, Ghana - 15/12/2010.Wananchi wa Ghana kwa mara ya kwanza wameungana na nchi nyingine dunia katika kuzalisha mafuta kutoka kwenye Ghuba ya Guinea.
Akifungua kuanza kwa uzalishaji huo rais wa Ghana John Atta Mills alisema "kuzalishwa kwa mafuta hayo ni baraka na siyo laaana kwa wananchi wa Ghana, na mafuta yatakayo patikana yataisaidia Ghana kuinua uchumi wake zaidi kulio ilivyo sasa."
Kiasi cha mapipa 55.000 yanatarajiwa kuzalishwa kwa siku.
Eneo hilo liligunduliwa kuwa linamafuta miaka mitatu iliyo pita na kampuni moja ya Uingreza Tullow Oil PLC.
Picha hapo juu ni ya ramani ya nchi ya Ghana ikiwa imefunikwa na rangi za bendera ya nchi hiyo ambayo kwa sasa inatambulika rasmi kuwa mzalishaji wa mafuta na kujiungana na nchi nyingine zilizopo katika bara la Afrika.
Wanasiasa maarufu Kenya wahusishwa katika machafuko ya 2007
Posted by
Kibatala
at
Wednesday, December 15, 2010
0
comments
Mahakama ya kubali maombi ya dhamana ya Julian Assange.
London, Uingereza - 14/12/2010. Mahakama jijini London imekubali kumwachia kwa masharti mwanzilishi wa mtandao wa Wiki Leaks kwa dhamana ya dola za Kiamerika $ 317,400.
Nairobi,Kenya - 14/12/2010. Kundi la wanasheria nchni Kenya wametishia kuandika barua kwa bunge la Kenya kufuta uanachama wake katika Mahakama ya Kimataifa (International Criminal Court-ICC).
Kundi hilo la wanasheria walisema " tulitaka haki itendeke na mahakama ya kimataifa lakini haikuwa hivyo kutokana na uchunguzi wao. Na tunaangalia ni njia gani tutatumia kupitia bunge kujitoa katika matakaba wa Roma ( RomeStatute)."
Mjadara huo umekuja baada ya ICC kusema inamajina sita ya watu waliohusika kuleta machafuko ya kisiasa kabla na baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika 2007.
Machafuko hayo yalisababisha vifo vya watu zaidi ya 1500 na wengine 300,000 kuachwa bila makazi.
Picha hapo juu anaonekana mmoja wa kijana akikimbia kuepusha maisha yake kutokana na machafuko yaliyo tokea kabla na baada ya uchaguzi nchini Kenya 2007 ambapo hali ya kiusalama ilikuwa imechafuka, kutisha kwa kilahali.
Waziri mkuu wa Itali ashinda kura za maoni kwa mara nyingine.
Roma, Itali - 14/12/2010. Waziri mkuu wa Itali ameshinda kura za maoni ambazo zilikuwa zimeitishwa zidi yake kutokana na baadhi ya wabunge na viongozi wa serikali kutokwa na imani naye.
Silvio Berlusconi,ameshida kura hizo za maoni kwa kiasi cha uchache wa kura dhidi ya wale wanaopinga uongozi wake.
Ushindi huo aliopata Berlusconi, siyo wa mara ya kwanza kwani alishida kura kama hiyo siku za nyuma.
Hata hivyo wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanasema Berlusconi atakuwa na wakati mgumu kuongoza serikali kutokana na upinzani mkubwa katika bunge na serikalini.
Picha hapo juu anaonekana waziri mkuu wa Itali,Silvio Berlusconi akionyesha dole baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa kuwa ameshinda tena kura za maoni ambazo ziliitishwa na vyama vya upinzani hivi karibuni.
Dunia ya mpoteza mtetezi wa amani.
Posted by
Kibatala
at
Tuesday, December 14, 2010
0
comments
Waziri mkuu wa Itali kuwekwa kenye boksi la maoni na wabunge.
Roma, Itali - 12/12/2010. Wachunguzi wa serikali wameanza uchunguzi kufuatia kuwepo na habari ya kuwa waziri mkuu wa Itali ametoa milungula ili ashinde kura za maoni kuuhusu uongozi wake.
Malalamiko hayo yalifunguliwa na kiongozi wa upinzani Antonia Di Puerto ambaye akikosoa uongozi wa waziri mkuu wa sasa Silvio Berluscon.
Naye kiongozi mwingine wa chama cha upinzani Luigi De Magistris alisema "tumeona rushwa inatumika kati ya wabunge ili kumuunga mkono Berluscon."
Hata hivyo Berluscon alisema "sidhani kama kutakuwa na wasaliti wengi na naimani serikali itashinda."
Uamuzi wa kutaka kura za maoni zipigwe kumekuja kutokana na baadhi ya wabunge hasa wa upande wa upinzani kutokuwa na inami na waziri mkuu kutokana na habari za matukio ambayo yanamuhusisha moja kwa moja.
Picha hapo juu ni picha waziri mkuu wa Itali, Silvio Berluscon ambaye serikali yake imekuwa na mvutano sana na vyama pinzani na kutaka kura za maoni zipigwe zidi ya uongozi wake.
Tokyo, Japan - 12/12/2010. Serikali ya Japan inajiandaa kuweka mitambo ya kuzuia
Washington, Amerika 12/12/2010. Wabunge wa chama cha Republikan nchini Amerika wamepinga mswaada wa serikali kutaka kutoa malipo ya huduma za kiafya kwa wale wote walio athirika wakati wa mashambulizi ya Septemba 11/2001.
Kwa mujibu wa habari zilizo patikana zinasema "kukataliwa kwa maswaada huo wa kuwasaidia malipo ya kiafya kutawaathiri pia wafanyakazi waliokuwa wanafanya kazi katika eneo hilo na wakazi wa vitingoji vya karibu na Ground Zero."
Tangu tukio la Septemba 11/2001, wanasiasa wamekuwa wakipishana kimawazo kuhusu swala hili.
Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya wafanyakazi wakiwa katika harakati za kusafisha mabaki ya majengo yaliyo bomoka, mara baada ya kulipuliwa na ndege zilizo tekwa nyara na magaidi.
Posted by
Kibatala
at
Sunday, December 12, 2010
0
comments